BIASHARA YAKO KUWA NA POOR PERFOMANCE

 Kuna siku nimekaa sehemu moja ya chakula, kisha akaja mhudumu akanambia nikusaidie nini, nikamwambia nataka chakula mną nini


Akanambia mbuzi, nyama Choma mishkaki ugali chips nk

Nikasema naomba nyama na ugali na Maji pls

Akasema naomba Hela kabisa nikasema Naomba lipa namba

Akasema kaka hapa cash mambo ya simu haturuhusu na sikuwa na Hela cash nikauliza kuna AtM hapa? Akasema iko mtaa wa pili nikaona sio mbaya wacha nikatoe Hela nije kula

Baada ya kutoa Hela narudi nakutana na Bango hapo hapo linasema “wakala wa bank, lipa kwa simu mpesa airtel tigo nk

Mmh nikauliza yule dada “sasa dada kumbe hapa mnaruhusu kulipa kwa simu! Mbona umenichosha hivyo!?

Akasema mimi sivielewi naona tu unipe Cash

Niliboeka sana na mood ya kula iliisha woooiiii

Nikasema ahsante

Ila nilicho notice Yule hana shida shida ni ma boss Żake wanajifunza wao ila hawafundishi staff wao

Na wewe 2024 hili kosa achaaaaaaa!!!

Comments